Habari

SERIKALI YATAKIWA KULEGEZA MASHARTI YA MIKOPO……………….

Serikali imetakiwa kulegeza masharti ya kuchukua mikopo hasa kwa vijana wanaotuma maombi bila mafanikio.

Afisa wa masuala ya mikopo kaunti ya Kwale Justus Mwaro amesema kuwa masharti yaliyowekwa na serikali ni magumu kwa vijana wanaotaka kuchukua mikopo hiyo.

Akizungumza katika eneo la Diani, Mwaro ameitaka serikali kutoa hamasa za kutosha kwa vijana kuhusu jinsi wanavyoweza kupata na kulipa mikopo hiyo kwa urahisi.

Kando na hayo, afisa huyo amedai kwamba baadhi ya maafisa wa serikali wanaotoa mikopo hiyo wamezembea kazini.

Aidha, Mwaro amewashauri vijana wanaopata mikopo hiyo kuitumia kwa malengo waliyokusudia.

 

By News  Desk