HabariSiasa

Idara ya mahakama yatajwa kama kikwazo kwa utekelezaji wa miradi ya hapa nchini………

Katibu katika wizara ya nyumba Charles Hinga ametaja idara ya mahakama kama mojawapo ya vikwazo vinavyotatiza baadhi ya miradi inayonuiwa kutekelezwa hapa nchini hasa ujenzi wa nyumba

Akizungumza mjini Mombasa katika mtaa wa Baxton Hinga amewataka wakaazi wa Mombasa kuunga mkono mradi huo alioutaja kama mojawapo ya miradi mikuu humu nchini.

Ameongezea kuwa mradi huo ni mkubwa ukilinganishwa na miradi nyingine nchini

Hata hivyo, Hinga amesema kuwa mradi huo unaolenga ujenzi wa takriban  nyumba 2,000 za kisasa unaweza kuchelewa kwa zaidi ya miaka 3 kufuatia mzozo ulioishia mahakamani.