HabariSiasa

Otiende Amollo asema alijiuzulu kabla ya kutimuliwa kutoka kwa kamati ya sheria bungeni………..

Mbunge wa Rarieda Otiende Amollo amesema kuwa alijiuzulu kabla ya baadhi viongozi wa ODM kuamua kumtimua kutoka kwa kamati ya sheria bungeni.

Otiende aidha amesisitiza kuwa hakuna mzozo wowote wala tofauti zozote baina yake na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga,

Hata hivyo Otiende amekanusha madai ya hapo jana  ya mwenyekiti wa chama cha ODM John Mbadi, kwamba alimtumia kinara wa ODM Raila Odinga ujumbe mfupi wa kutoa vitisho, Otiende amesema kuwa siku zote yeye humtumia Raila jumbe nyingi kwa sababu yeye ni wakili wake.

Aidha Otiende ameitaka tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kuchapisha matangazo kuhusu usajili wa wapiga kura unaoendelea kote nchini akisema utasaidia kwa wakenya wengi kujitokeza kusajiliwa.

By Joyce Mwendwa