BurudaniEntertainment

DOGO RICHIE: SIJAPENDEZWA NA ALICHOKIFANYA HAPPY C!!!

Baada ya msanii Dogo Richie kuonekana akifanya kazi ya Bodaboda watu wengi walitoa hisia zao akiwemo msanii Happy C kutoka 001 Music aliyetupia picha ya mchekeshaji kutoka Bongo Pierre akila bata kwenye mtandao na kuiambatanisha na caption iliosema (kabla ya Bin Laden hajakuwa Bodaboda)

Post hio haikupokelewa vyema na Dogo Richie na akaamua kupost akisema (Smts ni vigumu mtu kuelewa, sikutegemea post hii kutoka kwa Happy C. Hakuna mtu asiyependa maisha mazuri hata wewe ningekwambia unisaidie haungenisaidia kila siku, pili Mungu kakupa nafasi 001 of which nafurahi sana uwe sehemu uliopo sasa, Rafiki mwema ni yule wakusitiri mwenzake anapopata matatizo, hakuna anayejua kesho yake, familia yanitegemea, lazima waishi wasome, sijafil poa, napost hii but nimejifunza pia…)

By Leon Nkaduda.