BurudaniEntertainmentMombasa

NYOTA NDOGO YA AJAB!!!

Msanii mkongwe kutoka Mombasa kwa jina Mwanaisha Abdalla almaarufu Nyota Ndogo hapo jana katika mtandao wake wa instagram alipost picha akishukuru mashabiki wake na kwamba amekuwa mwanafamilia wa unga wa AJAB kutoka Grain Industries Limited.

Nikimnukuu “Kwa Kweli Mungu Huskia na Hujibu Maombi…. Leo imekua siku ya Furaha kwangu Saanaaaaaa…

Kwanza nitoe Shukran zangu Kwenu Mashabiki kwa kweli mumekua watu wakunisupport sana… Niliwaomba mutag Kampuni ambazo natumia Bidhaa zao kwenye Kupika… Ningependa kuwajulisha kwamba nimekua Mwana Familia wa UNGA WA @ajab_flour

Asante sana Mkurugenzi wa Kampuni ya AJAB…

Asanteni sana Mashabiki Zangu…

NAWAPENDA SANAAAAA???

DEAL SIGNED!!!!!?????? nikepewa unga bandali kwa mabandani Yani @nyotandogo_jikoni ndio nimeshasahau kununua unga hivi”

Wengi walimpongeza kupitia comment section akiwemo msanii Vivianne_ke akisema “Hongera mum ?” .

By Leon Nkaduda