Shule ya upili ya Sheikh Khalifa kutoka hapa mjini Mombasa ndio imeibuka bora katika kaunti ya Mombasa kwenye matokeo ya mtihani wa kidato cha nne wa mwaka 2020 baada ya mwanafunzi wa kwanza wa shule hio Asia Abubakar kupata gredi ya A ya alama 82.
Akiongea baada ya kupokea matokeo hayo naibu mwalimu mkuu wa shule hiyo sheikh Rishad Rajab amesema mbali na kupata alama hio ya A shule hio imepata A minus 29 B+ 59 na B- 59 nakushika nafasi ya 24 nchini.
Aidha ameelezea ushirikiano baina ya walimu, wazazi na wanafunzi ndio imechochea mafanikio hayo mema.
Kwa upande wake mwanafunzi Asia Abubakar ameweka wazi kuwa hakutarajia kupata matokea hayo japo alitarajia kufanya vyema.
Asia lengo lake ni kuwa daktari na angependelea kujiunga na chuo kikuu Cha Moi mjini Eldoret.
Miongoni mwa shule zilioandikisha matokeo bora hapa Mombasa, ni shule ya upili ya Light Academy, Shule ya Upili ya Istiqama na shule ya upili ya Qubaa Muslims.