HabariNewsSiasa

Gavana wa Wajir afika mbele ya kamati ya seneti kujitetea……….

Vikao vya kusikiza na kutathmini hoja ya kumbandua gavana wa Wajir Mohammed Abdi vinaendelea katika bunge la seneti.

Gavana Abdi amesomewa baadhi ya tuhuma zinazomkabili ikiwemo tuhuma za ufisadi, uvujanji wa sheria, ubadhirifu wa mali ya umma  na utumizi mbaya wa mamlaka.

Kamati maalum inayoongozwa na Seneta wa kaunti ya Nyamira Okongo Mogeni inatarajiwa kuandika ripoti yake ijumaa kabla ya kuwasilishwa kwa bunge la seneti tarehe 17 mwezi huu. Gavana Abdi anatarajiwa kujitetea dhidi ya tuhuma zilizosababisha kubanduliwa kwake.

Itakumbukwa kuwa wawakilishi wodi walimbandua gavana Abdi wiki mbili zilizopita.

By Joyce Mwendwa