HabariKimataifaSiasa

Museveni aapishwa rasmi kuhudumu kwa muhula wa sita……

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameapishwa rasmi kuwa rais wa Uganda kwa muhula wake wa sita huku usalama ukiimarishwa pakubwa katika hafla hiyo.

Hafla ya kuapishwa kwake imeandaliwa jijini Kampala ambapo viongozi wa nchi mbali mbali wamehudhuria ikiwemo  Tanzania, Burundi, Sudan Kusini na Somalia.

Askari wamezunguka nyumba ya Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine, ambaye alikuwa mshindi wa pili wa uchaguzi. Museveni ataiongoza Uganda kwa miaka mengine mitano.

Aliingia madarakani Januari 1986 kwa mapinduzi ya kijeshi, hadi utakapofika uchaguzi mwingine 2026 atakuwa madarakani kwa miaka 40, sawa na miongo minne.

Alishinda uchaguzi wa Januari 14, 2021 kwa kuwabwaga wagombea wengine kumi katika nafasi ya Urais kwa ushindi wa asilimia 58 ya kura zote.

Japo wapinzani nchini humo pamoja na waangalizi wa kimataifa na makundi ya haki za binaadamu kudai kuwa uchaguzi huo uliingiliwa na serikali ya Museveni na kuminya wagombea wa upinzani.

Siku ya Jumatatu, polisi walisema zaidi ya watu 40 walikamatwa kwa kupanga kuvuruga sherehe hiyo.

By Reporter Warda Ahmed