Habari

Vijana wanaotekeleza uhalifu Shimbahills waonywa vikali…..

Idara ya usalama kaunti ya Kwale imewaonya vikali vijana wanaotekeleza visa vya uhalifu katika msitu wa Shimba Hills kwenye barabara kuu ya Kwale-Kinango.

Kamishna wa Kwale Joseph Kanyiri ametoa onyo hilo kwa vijana wanaodaiwa kuwashambulia wahudumu wa magari na wasafiri wanaotumia barabara hiyo.

Kamishna huyo ameahidi kukabiliana na vijana hao wanaoaminika kujificha katika msitu huo ambapo wanatekeleza visa vya wizi.

Kanyiri ameeleza kwamba tayari maafisa wa polisi wanawandama  vijana hao waliojihami kwa silaha hatari.

By Kwale Correspondent