Habari

Serikali ya Kilifi kutumia milioni 8 kujenga daraja huko Jambiani……

Serikali ya kaunti ya Kilifi inalenga kutumia jumla ya shilingi milioni 8 katika ujenzi wa daraja huko Jambiani wadi ya Gongoni eneo bunge la Magarini.

Kulingana na Mwakilishi wa wadi hiyo Albert Kiraga wakaazi maeneo ya Kijandoni, Ondo na Jambiani wamekuwa na changamoto ya kuvuka mto wa Kinyaule hadi ng’ambo ya pili wanapotekeleza shughuli zao.

Kulingana na Kiraga, tayari ujenzi wa mradi huo kwa sasa umefikia asilimia 80.

Aidha kiongozi huyo ameelezea matumaini yake kwamba asilimia kubwa ya wanafunzi eneo hilo watapata  fursa ya kuhudhuria masomo yao kikamilifu baada ya mradi huo kukamilika kinyume na hali ilivyo kwa  sasa.

Maelfu ya wenyeji eneo hilo ambao ni wakulima pamoja na wafanyibiashara watapata afueni endapo ujenzi wa daraja hilo utakamilika.

By Correspondent Joseph Yeri