Uncategorized

Rais kufungua rasmi bandari ya Lamu, huku akihimizwa kuzungumzia suala la fidia……..

Rais Uhuru Kenyatta sasa ameshinikizwa kulizungumzia suala la fidia kwa wakaazi ambao wameathiri na ujenzi wa mradi wa bandari ya Lamu wa LAPSET wakati atakapozindua rasmi shughuli za bandari hiyo hii leo.

Katika taarifa yake mbunge wa Lamu Mashariki Shariff Athman amesema kuwa ipo haja kwa vijana kunufaika na mradi huo wa bandari huku pia akihimiza serikali kuwafidia kikamilifu walioathirika kutokana na ujenzi wa bandari hio.

Aidha ameitaka serikali kukamilisha karo ya vijana waliowapeleka vyuoni kusomea taaluma mbali mbali ili waweze kupata vyeti vyao vitakavyowawezesha kuajiriwa bandarini humo.

Athman amewasihi vijana kutokuwa na jazba kwa kisingizio cha kutoajiriwa kwani kama viongozi wanafanya mazungumzo na wakuu serikalini kuhakikisha ajenda yao ya kuajiriwa kwa vijana hao inatiliwa maanani.

Meli ya kwanza yenye shehena inatarajiwa kutia nanga kwenye bandari hiyo hii leo.

By Warda Ahmed