HabariWorld

Idadi ya wakimbizi wa ndani duniani yafikia milioni 55………

Idadi ya wakimbizi wa ndani kote duniani imefikia milioni 55.

Idadi hiyo iliongezeka zaidi mwaka jana kutokana na sababu mbali mbali.

Kulingana na ripoti ya kituo cha Internation displacement Monitoring centre IDMC na baraza la wakimbizi la taifa la NORWAY, vita na majanga ndio vilivyochangia hali hiyo licha ya kuwepo kwa masharti ya kudhibiti maambukizi ya corona katika mataifa mengi.

Kulingana na ripoti hiyo, watu milioni 40.5 walitoroka makaazi yao, ikimaanisha kwamba idadi hiyo ni ya juu zaidi kuwahi kuripotiwa kwa kipindi cha mwaka mmoja

By Warda Ahmed