HabariSiasa

IEBC yawasilisha notii ya kukata rufaa uamuzi wa mahakama kuu kuhusu BBI…….

Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini imewasalisha notisi ya kukataa rufaa uamuzi wa mahakama kuu kuhusu mswada wa marekebisho ya katiba kupitia ripoti ya BBI.

IEBC  inataka mahakama ya rufaa  kuangazia uamuzi wa majaji watano kuhusu uwezo wa IEBC kuendesha zoezi hilo kutokana na idadi isiyotosha ya makamishna.

Aidha tume hiyo ya uchaguzi inapinga uamuzi wa Mahakama kuu kwamba ilifaa kuendesha usajili wa wapiga kura na pia kueka mfumo wa kuhakiki saini ambazo zilizikusanyawa ili kuwezesha mswada wa BBI kujadiliwa katika mabunge ya kaunti.

 

By Joyce Mwendwa