AfyaHabariMombasaSiasa

Joho apinga madai kwamba dozi zilizosalia za Astrazeneca zitaharibika…….

Gavana wa kaunti ya Mombasa Hassan Joho amepinga vikali baadhi ya madai kwamba huenda takriban dozi elfu 2 za chanjo ya Astrazeneca ambazo zimesalia zikaharibika kabla hazijatumiwa.

Madai hayo yamekuwa yakiibuliwa baada ya serikali ya kaunti ya Mombasa kuanzisha mpango wa kuwachanja washikadau wa sekta ya utalii.

Gavana Joho amesema dozi hizo ziko salama na wala hazitaharibika kama inavyodhaniwa.

Ikumbukwe kwamba kaunti ya Mombasa ilipata jumla ya dozi elfu 30, 157 za astrazeneca na kufikia sasa zaidi ya watu 26,867 wamechanjwa.

 

BY NEWSDESK