AfyaHabari

Kampeni ya Chanjo ya polio dhidi ya watoto kuanza jumamosi hii……..

Wizara ya afya inatarajiwa kuanza kampeni ya kuwachanja watoto walio chini ya umri wa miaka mitano dhidi ya ugonjwa wa kupooza maarufu polio.

Awamu ya kwanza ya kampeni hiyo itaanza siku ya jumamosi huku watoto milioni 3.4 wakilengwa.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amepongeza mikakati iliyowekwa kukabili ugonjwa wa polio.

Katika hotuba iliyosomwa na Dkt Francis Kuria, Kagwe amesema kwamba Kenya na mataifa mengine yameweka mikakati kuhakikisha polio imekabiliwa, haswa ikizingatiwa kwamba ni mataifa mawili pekee Pakistan na Afghanistan ambayo bado yanahangaishwa na ugonjwa huo.

Ikumbukwe kwamba mwezi februari mwaka huu wizara ya afya ilithibitisha virusi vya polio katika maji taka kutoka maeneo ya Garissa na Mombasa, vile vile kaunti 13 ziko kwenye hatari ya kupata polio, kaunti hizo ni Mandera, Isiolo, Wajir, Garissa, Lamu, Tanariver, Mombasa, Kitui, Machakos, Nairobi, Kajiado na Kiambu.

Kagwe aidha amesema kwamba chanjo hizo zimethibitishwa kuwa ni salama.

BY NEWS DESK