Habari

Wizara ya elimu ina deni la takriban shilingi bilioni 7 la wachapishaji vitabu………….

Imebainika kuwa wizara ya elimu ina deni la takriban shilingi bilioni 7 la wachapishaji vitabu vya mfumo mpya wa elimu.

Kulingana na afisa mkuu mtendaji katika taasisi ya kubuni mtaala wa elimu nchini KICD Profesa Charles Ochieng Ogondo, kufikia sasa vitabu vya shilingi bilioni 30 vimesambazwa shuleni na kuwa wanajizatiti kuwalipa wachapisaji hao.

Akizungumza mbele ya kamati ya bunge la seneti kuhusu Elimu, Ogondo amesema hana ufahamu kuhusu iwapo baadhi ya shule nchini zina deni la wachapishaji waliokuwa wanauza vitabu kabla ya idara ya Elimu kuchukua jukumu la kusambaza vitabu shuleni.

Aidha Ogondo amewahakiishia maseneta kuwa kila shule itapata vitabu kwa mujibu wa idadi ya wanafunzi katika shule hizo kwani kuna mikakati ya kusambaza vitabu vya Grade 5 kabla ya wanafunzi kufungua shule mwezi Julai.

By Joyce Mwendwa