Habari

Mamlaka ya mawasiliano nchini yapongeza vyombo vya habari………

Vyombo vya habari nchini vimepongezwa kwa kupeperusha taarifa zilizothibitishwa na ambazo ni za kuelimisha jamii.

Kaimu afisaa mkuu mtendaji wa mamlaka ya mawasiliano nchini CA Mercy Wanjau amedokeza kwamba zaidi ya asilimia 95 ya wakenya wanatambua kuwepo kwa virusi vya corona kupitia taarifa za vyombo vya habari.

Wanjau aidha anasema virusi hivyo vimechangia pakubwa kupungua kwa mapato katika sekta ya uanahabari na mamlaka ya CA imekuwa ikishirikiana na mashirika mbali mbali ya habari katika kupunguza matozo ya kila mwaka.

Ameyasema hayo katika hafla ya kutangaza matokeo ya tuzo za kuza mwaka huu.

By Warda Ahmed