HabariMombasa

CHAMA CHA KNUT TAWI LA MOMBASA KIMETOA MWONGOZO UTAKAO TUMIKA KATIKA UCHAGUZI MKUU….

Chama cha kutetea maslahi ya walimu nchini tawi  la mombasa KNUT kimetoa mwongozo utakao tumika katika uchaguzi mkuu wa chama hicho katika ngazi ya juu baada ya kuwasilisha majina ya watakao peperusha ajenda ya walimu katika ukanda wa Pwani………..

Akizungumza na meza yetu ya habari baada ya kuchaguliwa kama mwenyekiti wa chama hicho katika kaunti ya Mombasa kwenye hoteli ya Red Bidge mjini mombasa, David Mulei ameeleza matumaini yake kwamba kikosi hicho ambacho kimechaguliwa katika mkutano huo kitatwa ubingwa katika uchaguzi mkuu wa KNUT huku akisisitiza kuwa chama hicho kiko imara.

Kwa upande wake Dan Aloo ambae ameidhinishwa na chama hicho tawi la mombasa kuwania kiti cha  mwenyekiti katika ngazi ya juu amesema kwamba anamatumai kuwa chama hicho kitasalia imara licha ya kupigwa vita na tume ya kuajiri walimu nchini TSC, Aloo aidha  amehimiza serikali kutoa fedha ili kuimarisha chama hicho , huku akitangaza msimamo wake kuunga mkono Wilson Sossion kama katibu mkuu wa KNUT.

Kadhalika Magarete kenga ambae ameteuliwa kama  mwakilishi wa kina mama katika chama hicho amesisitiza chama hicho kuwa imara licha ya msukko  msuko unaoshuhudiwa.

By David Otieno