HabariMichezo

ALIYEKUWA KOCHA WA ZAMANI WA TIMU YA RAGA YA RUGBY SEVENS BENJAMIN AYIMBA AAGA DUNIA.

Rais Uhuru Kenyatta  ametuma risala za rambirambi kwa familia jamaa na marafiki wa  aliyekuwa kigogo  wa  mchezo wa Raga na  pia kocha wa zamani wa timu ya Raga ya Rugby Sevens, Benjamin Ayimba ambaye alifariki jana jioni katika hospitali ya Nairobi alipokuwa anapokea matibabu ya ugonjwa wa Malaria.

Rais Kenyatta amemtaja Ayimba kama shujaa katika mchezo wa Raga na ambaye aliwahamasisha wakenya wengi kujiunga na kuboresha mchezo huo.

Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga na yule wa Wiper Kalonzo Musyoka ni miongoni mwa viongozi wa kisiasa waliotuma jumbe zao za rambirambi.

Raila amemtaja mwendazake kama mzalendo aliyefanikisha mengi nchini katika Nyanja za michezo. Kwa upande wake gavana wa kitui Charity Ngilu amemkumbuka katika michuano aliyoyaandaa kwa ushirikiano wa serikali ya Kitui.

BY KHADIJA BINTIMZEE