HabariSiasa

Wanasiasa wahimizwa kuiga mfano wa jaji Koome na Jaji Willian Ouko……..

Jaji wa mahakama ya juu Martha Koome amewataka wanasiasa kuiga mfano wake na mwenzake Jaji William Ouko kuhusu ushindani usiokuwa na uadui.

Akizungumza baada ya kukaribishwa na kaimu mwenyekiti wa tume ya idara ya mahakama JSC proffesa Olive Mugenda, Jaji Koome ameeleza jinsi walivyotiana moyo kwanza wakiwania wadhfa wa jaji mkuu, kabla ya jaji William Ouko baadaye kupata wadhfa wa jaji wa mahakama ya juu.

Ikumbukwe wawili hao walikuwa kwenye darasa moja katika chuo kikuu cha Nairobi.

By Warda Ahmed