HabariSiasa

Rais amtaka jaji Koome kutekeleza majukumu yake kwa haki…………

Rais Uhuru Kenyatta ameeleza kufarahishwa kwa kuidhinishwa kwa jaji mkuu mpya akisema ni heshima kwake kuwa rais wa kwanza kumuapisha jaji mkuu wa kwanza mwanamke humu nchini.

Jaji Martha Koome ni jaji mkuu wa kwanza mwanamke nchini na vilevile rais wa Mahakama ya juu zaidi.

Rais Kenyatta aidha amemtaka jaji Martha Koome kutekeleza majukumu yake kwa uaminifu na kwa haki akiongezea kwamba watashirikiana pamoja.

Hafla ya kuapishwa kwake imeandaliwa katika ikulu ya rais jijini Nairobi.

BY Joyce Mwendwa