BurudaniHabari

Machifu wahimizwa kukomesha disco matanga huko Kwale………

Idara ya usalama kaunti ya Kwale imewaagiza maafisa wa serikali ya utawala kuhakikisha hakuna hafla za disco za usiku zinazofanyika kaunti hiyo.

Kamanda wa polisi kaunti ya Kwale Ambrose Steve Oloo amewataka machifu na wazee wa mitaa pamoja na mabalozi wa nyumba kumi kudhibiti disco hizo.

Oloo amesema kuwa ni kinyume na sheria kucheza disco kwa kuwa inakiuka sheria za wizara ya afya za kukabiliana na ugonjwa wa virusi vya corona.

Kamanda huyo amewaonya pia wale wanaocheza disco hizo nyakati za usiku kwamba watachukuliwa hatua za kisheria.

Afisa huyo wa polisi amebainisha kuwa visa hivyo vimekithiri mno katika maeneo bunge ya Kinango na Matuga.

By Kwale correspondent