HabariMombasa

Waumini wa kikristo wanaokwenda kwa waganga wakemewa vikali……..

Mchungaji  wa kanisa Jesus Victory Joel Masika kaunti ya Mombasa amekemea tabia ya  waumini wa dini ya Kikristo katika ukanda  wa Pwani kuenda kwa waganga ili kutafuta suluhu la matatizo yao.

Akizungumza na meza yetu ya habari, mchungaji Joel amekitaja kitendo hicho kuwa kinyume na imani ya kikristo.

Masika amesema kwamba ni hali ya kusikitisha kuwaona  waumini  ambao wanapaswa kuiweka imani yao kwa Mungu na kumuomba bila kuchoka wanachukua maamuzi ya kutafuta msaada kwa waganga.

Aidha mchungaji Joel ameelezea athari zinazoshuhudiwa baada ya Wakristo kutafuta suluhu la matatizo yao kwa waganga huku akisema tabia hizo zinaenda kinyume na neno la Mungu kwenye kitabu kitakatifu.

By Warda Ahmed