AfyaHabari

KENYA YAANZA HARAKATI YA KUTAFUTA CHANJO MBADALA YA COVID-19……..

Kenya imeanza harakati ya kutafuta chanjo mbadala kufuatia changamto zilizoibuka katika usafirishaji wa chanjo ya AsrtaZeneca

Wanasayansi katika taasis KEMRI kaunti ya Busia wameanza mikakati ya kutayaharisha stakabadhi zitakazowapa nafasi ya kuchunguza chanjo mbadala.

Utafiti wa chanjo hizo kutoka Kenya na Uchina zitaanza miezi michache ijayo.

Taasis ya KEMRI ilihusika katika utrafiti wa ubora wa chanjo ya Astrazeneca kwenye bewa la Kilifi kabla ya kuruhusiwa kutumika nchini.

Raia kati ya 60 hadi 100 wanatarajiwa kuhusika kwenye awamu ya kwanza ya majaribio ya chanjo hizo mbadala.

Wizara ya afya inasubiria chanjo ya Astrazeneca kutoka mataifa jirani ili kuhakikisha waliopata chanjo ya kwanza wanadungwa ya pili na kuwapa kinga inayostahili dhidi ya Corona.

Haya yanajiri huku serikali za kaunti zikitakiwa kuboresha huduma zake katika hospitali zinazopambana na maradhi ya Covid 19

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema mkumbu wa nne wa Corona unatarajiwa majuma machache yajao.

BY JOYCE MWENDWA