HabariMombasa

UJENZI WA UWANJA WA FRERE TOWN WAKUMBWA NA MKANGANYIKO….

Viongozi, wazazi pamoja na usimamizi wa shule ya msingi ya Frere town katika eneo bunge la Nyali katika kaunti ya Mombasa wamekinyooshea kidole cha lawama serikali ya kaunti ya Mombasa kwa madai ya kuzuia ujenzi kwenye uwanja wa shule hio.

Wakiongozwa na mbunge wa eneo hilo Mohamed Ali, licha hata baada ya hazina ya CDF eneo bunge la Nyali kutenga takriban shilingi milioni 7 kwa ukarabati wa uwanja huo, juhudi hizo zimegonga mwamba baada ya serikali ya kaunti ya Mombasa kudidimiza mpango huo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya shule hio Samuel Karama amesema kwamba haja yao ni ujenzi kwenye uwanja wa shule hio huku akiongezea kwamba uwanja huo umgeuka na kuwa uwanja wa waraibu wa dawa za kulevya.

BY NICK WAITA