AfyaHabari

Wanaume washauriwa kuvunja kimya na kuunga mkono juhudi za hedhi salama na kwa wasichana na wanawake.

Wanaume wameshauriwa kuvunja kimya chao na kuunga mkono juhudi za kufanikisha hedhi salama na kukabiliana na changamoto za hedhi kwa wasichana na wanawake.

Kulingana na Mwaanzilishi wa kikundi cha vijana cha DADIMA 006 huko kaunti ya Taita Taveta Rogers Ngoo amesema kuwa wanaume wanaweza kushirikishwa katika maswala ya uwekezaji, ununuzi wa bidhaa hitajika kama vile sodo.

Ameongeza kuwa asilimia kubwa ya viongozi wanaofanya maamuzi katika serikali na nyanja mbali mbali ni wanaume hivyo ni vyema kutumia nafasi zao kubuni sheria na kufanya maamuzi ya kuwekeza zaidi katika maswala ya hedhi nchini.

Kwa upande wake mwanaharakati kutoka shirika la Taita Taveta Human Rights Watch Beatrice Mjomba amesema kuwa kuna haja ya kuweka miundo msingi katika shule zote za umma na maeneo ya umma ili kuwepo na mazingira salama kwa wasichana wakati wao wa hedhi.

Haya yanajiri huku  ulimwengu hapo jana ukiadhimisha siku ya hedhi salama huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni hatua na uwekezaji kwa usafi na afya ya hedhi huku wito ukizidi kutolewa kwa wanaume kuwa mastari wa mbele katika maswala ya uwekezazi.