HabariKimataifaSiasa

Mahakama ya Katiba ya Mali imemtangaza Kanali Assimi Goita kuwa rais mpya wa mpito nchini Mali……

Mahakama ya Katiba ya Mali imemtangaza Kanali Assimi Goita kuwa rais mpya wa mpito kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Rais Bah Ndaw ambaye amejiuzulu.

Katika uamuzi wake mahakama hiyo imesema Goita aliyeongoza mapinduzi ya kijeshi siku ya Jumatatu anapaswa kujaza nafasi hiyo.

Uamuzi huo unazidisha mkwamo ambapo viongozi wa mataifa ya Afrika Magharibi wakiwa wanajiandaa kukutana siku ya Jumapili kuzungumzia hatua ya kukabidhi madaraka, ambayo inahatarisha harakati za kuelekea kwenye demokrasia na kudhoofisha mapambano dhidi ya wapiganaji wa jihadi katika ukanda huo.

Goita alikuwa makamu wa rais baada ya kuongoza mapinduzi mwezi Agosti mwaka uliopita na kumuondoa madarakani Rais Ibrahim Boubacar Keita. Ndaw na Waziri Mkuu, Moctar Ouane ambao walishikiliwa baada ya mapinduzi hayo walijiuzulu siku ya Jumatano,wakiwa bado kizuizini.

 

By Khadija Binti Mzee