HabariMazingiraMombasa

Hatua ya waziri Najib Balala, yaendelea kuibua hisia mseto……..

Hatua ya waziri wa utalii na wanyamapori nchini Najib Balala, hapo awali kutoa pendekezo la kutaka ushirikiano wa kibinafsi katika mbuga za wanayama bado ingali inaendelea kuibua hisia mseto.

Mwakilishi wa wadi ya Kalolenyi kaunti ya Taita Taveta Christopher Mwambingu amesema iwapo hilo litafanikishwa,huenda likaathiri wakaazi wanaoishi karibu na mbuga hizo.

Mwambingu amesema huenda ikawa vigumu kwa wananchi wa kawaida kutembelea mbuga hizo kwani ushirikiano wa kibinafsi utabadili utaratibu wa shughuli za mbuga hizo za wanyama pori.

Hata hivyo waziri Balala hapo awali alieleza kuwa lengo la pendekezo hilo si la kubinafsisha mbuga za wanyama pori bali ni kutafuta mbinu za kuendesha shughuli hasa wakati huu ambapo janga la Covid-19 limeathiri sekta ya utalii.

Mahakama ya Katiba ya Mali imemtangaza Kanali Assimi Goita kuwa rais mpya wa mpito kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Rais Bah Ndaw ambaye amejiuzulu.

Katika uamuzi wake mahakama hiyo imesema Goita aliyeongoza mapinduzi ya kijeshi siku ya Jumatatu anapaswa kujaza nafasi hiyo.

Uamuzi huo unazidisha mkwamo ambapo viongozi wa mataifa ya Afrika Magharibi wakiwa wanajiandaa kukutana siku ya Jumapili kuzungumzia hatua ya kukabidhi madaraka, ambayo inahatarisha harakati za kuelekea kwenye demokrasia na kudhoofisha mapambano dhidi ya wapiganaji wa jihadi katika ukanda huo.

Goita alikuwa makamu wa rais baada ya kuongoza mapinduzi mwezi Agosti mwaka uliopita na kumuondoa madarakani Rais Ibrahim Boubacar Keita. Ndaw na Waziri Mkuu, Moctar Ouane ambao walishikiliwa baada ya mapinduzi hayo walijiuzulu siku ya Jumatano,wakiwa bado kizuizini.