Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir amewahakikishia watu wa Mombasa kwamba atakuwa kwenye kinyang’anyiro cha ugavana ndani ya kaunti ya Mombasa ifikapo uchaguzi wa 2022.
Akihojiwa na kituo kimoja cha radio, Abdulswamad anasema yuko na sababu ya kufanya hivyo baada ya kuwatumikia watu wa mvita kwa uaminifu mkubwa akisema sasa ni wakati wa kutazama siasa za kaunti.
Akijibu swali la kama yuko na shahada ya Degree kumuwezesha kuwania kiti hicho Abdulswamad amewasuta wapinzani wake aliowataja kwamba hawana habari zozote kuhusiana na maisha yake ya masomo, akisema watashangaa watakapoliona jina lake debeni.
By Warda Ahmed