Serikali ya kitaifa pamoja na ile ya kaunti ya Kilifi zimetakiwa kuwekeza zaidi katika usambazaji wa sodo sawia na mipira ya kondomu nchini.
Haya yanajiri baada ya kubainika kuwa serikali imeweka mbele usambazaji wa kondomu kuliko sodo nchini hivyo kusababisha changamoto kwa wasichana na wanawake wakati wa hedhi.
Ni jambo ambalo limeonekana kuwakera wadau wanaotetea haki za wanawake hasa katika kaunti ya Kilifi,wakisema kuwa serikali inatakiwa kuzingatia zaidi swala la athari za hedhi miongoni mwa wanawake na hata kuzifanya sodo kuwa bila malipo sawia na mipira ya kondomu nchini.
Aidha wasichana wengi katika kaunti hiyo ya Kilifi wanapata changamoto kubwa wakati wa hedhi anavyoeleza mwalimu katika shule ya msingi ya Chumani.
By Reporter Gladys Marura