HabariNewsSiasa

Raila amshutumu vikali aliyekuwa jaji mkuu Willy Mutunga…………

Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amemshutumu vikali jaji mkuu mstaafu Willy Mutunga kwa  kumshutumu rais Uhuru Kenyatta kufuatia madai ya kuhujumu idara ya mahakama.

Akizungumza katika hafla ya mazishi ya aliyekuwa mbunge wa Kibwezi Kalembe Ndile, Odinga amesema Mutunga mwenyewe hakuheshimu sheria.
Akiregelea kesi waliyowasilisha mahakamani ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2013, Raila amesema Mutunga alifutilia mbali kesi yao ilhali walishinda uchaguzi huo.

Wakati huo huo Raila amekariri kwamba Reggae ya BBI ingalipo.

Hafla ya mazishi ya marehemu Kalembe Ndile imeandaliwa nyumbani kwake huko kaunti ya Makueni.

By Nicky Waita