Habari

Hospitali nyingi ukanda wa pwani zinaKumbwa na uhaba wa damu…………………..

Shirika la msalaba mwekundu linasema hospitali nyingi ukanda wa pwani zinalumbwa na uhaba wa damu.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Malindi mshikishi wa shirika hilo Boniface  Mwaringa amefichua kuwa zaidi ya watu mia mbili wanahitaji damu kaunti ya Kilifi pekee kila baada ya lisaa limoja.

Mwaringa sasa anatoa wito kwa wakaazi mjini malindi kujitokeza kwa wingi na kutoa damu kwa vitengo husika ili kuokoa maisha ya maelfu ya wagonjwa hospitalini.

Kauli ambayo imeungwa mkono na mkurugenzi wa maswala ya kukusanya damu mjini Malindi Daniel Katana anayesema idadi kubwa ya wagonjwa wanaumia hospitalini kutokana na uhaba huo.

Katana amesema kitengo hicho kimejizatiti katika kuhakikisha kuwa wanaojitolea kutoa damu wananufaika siku za usoni endapo watakuwa na uhitaji wa damu.

By David Otieno