Habari

Hazina ya kitaifa kusambaza shilingi bilioni 39 kwa serikali za kaunti kufikia ijumaa…..

Hazina ya Kitaifa imesema kwamba itatoa Shilingi 39 bilioni kwa serikali za kaunti ifikapo Ijumaa wiki hii.

Akizungumza na maseneta mapema leo,  waziri wa fedha Ukur Yatani  amesema wizara yake itajitahidi kutoa fedha hizo ili kuwezesha kaunti kuweza kulipa madeni ya mwezi machi na Aprili.

Yatani amesema haya siku moja tu baada ya magavana kutishia kusitisha huduma kwenye kaunti zao Alhamisi ijayo iwapo hawatapokea pesa hizo kufikia Ijumaa.

Kupitia baraza la magavana, magavana hao walisema kwamba hazina ya kitaifa haijatoa shilingi bilioni 102 kwa kaunti zote 47 huku ikiwa ni wiki mbili tuu zimesalia ili mwaka huu wa fedha kukamilika.

Huyu hapa ni mwenyekiti wa baraza la magavana Martin Wambora akizungumza hapo jana.

 

By Nicky Waita