Serikali ya kaunti ya Kilifi inalenga kushirikiana na maafisa wa tume ya ardhi nchini ili kutatua mizozo ya ardhi kaunti hiyo.
Akizungumza na kituo hiki waziri wa ardhi kaunti hiyo Maurine Mwangovya amesema tayari Gavana wa Kaunti hiyo Amason Kingi ametoa muongozo wa nivipi maafisa wake watashirikiana na wale wa tume ya ardhi ili kutatua changamoto zinazoshuhudiwa kwa sasa.
Wakati uohuo Mwangovya amesema tayari ripoti kuhusu maeneo yenye changamoto imekamilika na huenda ikawasilishwa kwa gavana hivi karibuni kwa utekelezwaji.
Kauli yake inajiri baada ya mzozo kushuhudiwa katika mipaka ya Galana Kulalu kati ya wakulima na wafugaji.
By Joseph Yeri