HabariMombasa

Mwanamke anayehusishwa na mauaji ya msichana wa miaka 19 kufikishwa mahakamani……….

Mwanamke anayehusishwa na mauaji ya msichana mwenye umri wa miaka 19 anatarajiwa kusomewa mashtaka hii leo katika mahakama ya Mombasa.

Siku mbili zilizopita mahakama iliagiza mshukiwa huyo kwa jina Faiza Ali Hassan kuzuiliwa ili kutoa muda kwa mahakama kutafuta mkalimani wa lugha ya kisomali.

Uamuzi huo uliafikiwa na hakimu mkuu vincent Adet baada ya Faiza kudai kwamba haelewi lugha ya Kiswahili ama kiingereza.

Inadaiwa kuwa Faiza ndiye alikuwa mtu wa mwisho kuonekana na Najma Abdullahi kabla ya kupatikana akiwa amepoteza fahamu katika barabara ya Dongo Kundu hapa Mombasa.

Najma alifariki dunia muda mfupi baadae alipokuwa akitibiwa katika hospitali ya portreez kutokana na majeraha mabaya ya kichwa.

By Warda Ahmed