Serikali ya kaunti ya Mombasa ikishirikiana na washikadau wa mashirika kadhaa wanazindua kampeni ya kusafisha mazingira ya bahari ili kuokoa viumbe wa baharini.
Wakizungumza katika kongamano la uzinduzi huo, washikadau hao wanasema ni wakati sasa wa kuja na mikakati ya kuhakikisha mazingira ya bahari ni safi na salama baada ya kubainika kwamba takriban tani milioni 13 za plastiki hupatikana kila mwaka baharini.
Hatua hii husababisha jumla ya aina 800 wa viumbe baharini kuathirika na hata kufa ikwemo kasa, papa na aina nyinginezo za viumbe hao.
Nancy Githaiga ni afisaa wa shirika la WWF Kenya.
Kwa upande wao wenye kampuni za kuokota na kusafisha fuo za bahari kaunti ya Mombasa wameweka wazi kuwa jukumu lao kubwa ni kuhakikisha kuwa sehemu hizo zinakua safi kwa utalii na kuhakikisha usalama wa viumbe vya baharini.
Kongamano hilo limeandaliwa kwa ushirikiano wa serikali ya kaunti ya Mombasa na shirika la WWF.
By Warda Ahmed