HabariNews

Serikali Kwale kukusanya ushuru wa zaidi ya shilingi milioni 275……

Serikali ya kaunti ya Kwale inalenga kukusanya ushuru wa zaidi ya shilingi milioni 275 katika mwaka wa kifedha wa 2021/2022.

Waziri wa fedha kaunti hiyo Bakari Sebe amesema kwamba wanalenga kuongeza kiwango cha ushuru huo katika bajeti ya ziada.

Akizungumza eneo la Kinondo kaunti ndogo ya  Msambweni, Sebe amesema kuwa kuongezeka kwa kiwango hicho kutategemea pakubwa uchumi wa taifa.

Aidha, amesema kupungua kwa kiwango cha ushuru kutaathiri pakubwa matumizi ya serikali na miradi ya maendeleo kaunti hii.

Haya yanajiri wakati ambapo kaunti ya Kwale inadai serikali ya kitaifa zaidi ya shilingi bilioni 2.7 katika mwaka wa kifedha wa 2020/2021.

By Kwale Correspondent