HabariNews

Wakaazi Malindi watakiwa kupuuzilia mbali madai yanayotolewa na wanasiasa……

Wakaazi eneo bunge la Malindi wametakiwa kupuzilia mbali madai yanayotolewa na baadhi ya wanasiasa kuwa eneo bunge hilo litagawanywa mara mbili endapo hoja ya BBI itafaulu.

Akizungumza afisini mwake mshirikishi wa shughuli za uchaguzi eneo hilo Sudi Masha amesema madai hayo hayana msingi wowote kwani vigezo vinavyotumiwa kuongeza maeneo bunge haviko katika eneo bunge hilo.

Wakati uohuo afisa huyo amesema afisi yake inalenga kushirikisha afisi za utawala eneo hilo ili kuongeza idadi ya watu wanaojisajili kama wapiga kura.

Aidha amebainisha kuwa tume hiyo inalenga kuelekea nyanjani hata zaidi ili kutoa hamasa ya umuhimu wa wakaazi kujitokeza na kushiriki zoezi la upigaji kura.

Masha aliyasema haya kwenye zoezi lililozinduliwa la wiki ya kutoa hamasa kuhusu huduma mbali mbali za tume hiyo.

By Joseph Yeri