Habari

Spika wa bunge aunga mkono pendekezo la madaktari……

Spika wa bunge la kitaifa Justin Muturi anaunga mkono pendekezo la madaktari lakutaka kubuniwa kwa tume kuu ya kushughulikia maswala ya afya nchini

Akizungumza kwa njia ya mtandao katika kongamano la 48 la wanasayansi na madaktari katika kaunti ya Kisii, Muturi amesema kuwa tume kama  hii itachangia pakubwa kuzuia migomo ya mara kwa mara ya madaktari.

Muturi aidha ameongeza kwamba kubuniwa kwa tume hii kutasaidia kutatua migogoro ambayo imekuwa ikishuhudia kati ya serikali za kaunti na sekta ya afya chini ya miungano ya wahudumu wa afya

Amehimiza kamati zote kuu zinazojukumika na maswala ya afya katika seneti na bunge la kitaifa kushirikiana na madakatri ili kufanikisha mpango huo.

 

BY PRESTON ALLAN