Habari

Maafisa wa kliniki watishia kuandaa mgomo……………

Maafisa wa kliniki wametishia kuandaa mgomo kutokana kile wanachokidai kwamba ni ubaguzi wa huduma ya bima ya afya NHIF.

Maafisa hao wametoa makataa ya siku 7 kwa  bodi ya kusimamaia bima ya afya nchini, ili kuondoa hatua hiyo ambayo wanadai kuwa ni ubaguzi wa hali .

Chama cha madakatari pamoja na maafisa wa afya nchini KMPDU tayari kimewasilisha malalamishi yao katika mamlaka ya kusimamia bima ya afya nchini pamoja na wizara ya afya kupitia waziri wa afya Mutahi Kagwe wakisema kuwa iwapo wahusika hao watadinda kutekeleza matakwa yao watakwenda katika maandamano ya amani.

 

BY NATASHA SAGHE