AfyaHabari

Dozi elfu 358 za chanjo ya Astrazeneca kuwasili nchini leo usiku…….

Dozi elfu 358 za chanjo aina ya Astrazeneca zinatarajiwa kuwasili humu nchini leo usiku kutoka nchini Denmark.

Dozi hizo zinatarajiwa kupiga jeki awamu ya pili ya utoaji wa chanjo ambayo inaendelea japo kwa kujikokota kufuatia kutokuwepo kwa dozi za kutosha.

Kufikia wikendi wakenya elfu 188 walikuwa tayari wamepata chanjo ya pili.

Kufikia mwezi huu serikali ilikuwa imeahidi kwamba chanjo zaidi ya milioni 25 zingewasilishwa japo imekuwa vigumu kuafikia hitaji hilo.

 

By Warda Ahmed