HabariMombasa

KEMNAC yalaani hatua ya watu kupotea kiholela…..

Mwenyekiti wa baraza la waumini wa dini ya kislamu nchini KEMNAC nchini Sheikh Juma Ngao ameunga mkono hatua ya mwenyekiti wa IEBC kuwa viongozi waweze kuwa shahada ili waweze kuwania viti mbali mbali nchini.

Akizungumza na wandishi wa habari katika hoteli moja hapa Mombasa, Ngao amesema ni sharti viongozi waweze kuwa na elimu ya kutosha ili wawe na uwezo wa kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Kiongozi huyo amesema ni hatari kuwaruhusu viongozi wasio na elimu kusimamia miradi mbali mbali ambayo inagharimu fedha nyingi akisema hiyo inazidi kuchangia ufisadi nchini.

Wakati huo huo Ngao amelaani vikali hatua ya watu kupotea kiholela,huku akitoa wito kwa serikali kuu na za kaunti  kutoa taarifa kamili  kuhusu jambo hilo akisema hayo yanajiri kutokana na maafisa wa polisi  kuzembea kazini.

Ngao amesema kuwa viongozi wa kisiasa ndiyo wahusika wakuu kwani sio mara kwanza mambo kama hayo kushuhudiwa hasa uchaguzi unapokaribia.

Ngao ametoa makataa ya siku 7 kwa rais uhuru kenyatta kukemea unyama huo.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya idadi kubwa ya watu hasa watoto wa kike kupotea katika njia tatanishi.

 

By David Otieno