HabariMombasa

Viongozi wa dini ya kiislamu wadai TSC ina ubaguzi katika uajiri…….

Viongozi wa kidini kutoka baraza la waumini wa dini ya kiislamu nchini KEMNAC wamekashifu vikali tume ya kuajiri walimu nchini TSC kwa kille wanachokidai ni ubaguzi wa hali ya juu katika kuajiri walimu wa somo la kiislamu yani IRE.

Akizunguma na wandishi wa habari naibu mwenyekiti wa Kemnac Abubakar Amin amesema tume hiyo imekuwa ikitoa nafasi kwa walimu wakikristo na kuacha nje walimu wa kiislamu.

Abubakar aidha ameomba serikali kuzingatia hali hiyo na kuleta usawa katika ajira ya walimu nchini.

Wakati huo huo ametoa wito kwa serikali kuleta usawa katika uteuzi wa nyadhfa tofauti za serikali, akisema jamii ya kiislamu imeachwa nje katika uteuzi kwenye serikali.

Haya yanajiri huku kundi la wanaharakati wa kutetea haki za binadamu likiwasilisha kesi mahakamani kupinga takwa la wagombea wote wa kisiasa katika uchaguzi mkuu ujao kuwa na shahada.

Kwa mujibu wa wanaharakati hao, takwa hilo linawakandamiza wagombea mbali mbali hususan wawakilishi wadi ambao wanadai kwamba shahada inayopendekezwa haihitalifiana na utendaji kazi wao mashinani.

 

By David Otieno