Habari

Muda wa kuhudumu wa baraza la kitaifa la viongozi wa dini waongezwa…..

Muda wa kuhudumu wa baraza la kitaifa la kidini umeaongezwa hadi tarehe 31 ya mwezi desemba mwa huu.

Muda wa baraza hilo la kitaifa ulitarajiwa kukamilika hii leo.

Akitangaza mabadiliko hayo, waziri wa usalama wa ndani Fred Matiangi amesema wamechukua maamuzi hayo baada ya kufanya mashauriano na viongozi wa baraza hilo.

Baraza hilo linaloongozwa na kasisi wa kanisa katoliki Anthony Muheria limekuwa mstari wa mbele katika kukabili maambukizi ya virusi vya corona kwa ushirikiano na serikali.

Wakati uo huo Matiangi amewataka maafisa wa usalama kuimarisha uhusiano wao na viongozi wa dini akisema viongozi hao ni nguzo muhimu katika vita dhidi ya virusi vya corona.

Miongoni mwa mikakati ambayo imeachiwa baraza hilo ni kuhakikisha kwamba maeneo ya kuabudu yanitimiza mahitaji ya kisheria ya idadi ya watu, ikiwemo pia umbali wa watu na hata upimaji wa joto.

By Warda Ahmed