Habari

Hazina ya kitaifa yalitaka bunge la kitaifa kuidhinisha shilingi bilioni 45.5 zaidi……

Hazina kuu ya kitaifa imelitaka bunge la kitaifa kuidhinisha shilingi bilioni 45.5 zaidi ili kukimu bajeti ya mwaka 2021 mwaka unaokamilika mwishoni mwa mwezi huu.

Waziri wa fedha Ukur Yattani ameambia kamati ya bajeti bungeni kwamba fedha hizo zitatumika kuangazia zaidi mikakati ya kufufua uchumi kutokana na makali ya covid 19.

Akihutubu alipofika mbele ya kamati hiyo ambayo inaongozwa na mwenyekiti mbunge wa Kieni Kanini Kega, Yattani amesema kufikia sasa hazina hiyo imepokea ombi la shilingi bilioni 162.5 kutoka kwa serikali za kaunti ili kufanikisha utendaji kazi wao.

 

By Warda Ahmed