HabariSiasa

Mswada kuhusu dawa za kulevya kuregeshwa bungeni ili kuongezwa vipengee vikali zaidi……

 

Rais Uhuru Kenyatta ana mpango wa kurejesha mswada wa mwaka jana bungeni kuhusu dawa za kulevya, wakati huu ukiwa na vipengee zinazopendekeza adhabu kali zaidi.

Mbunge wa Lwanda Chris Omulele amepongeza hatua hii lakini kwa wakati huo akaomba mswada huo upigwe msasa ili uzingatie zaidi kumsaidia mraibu kurekebika kuliko kumuadhibu na kifungo.

Aidha Ted Odunga wakili wa mahakama kuu amesema kuwa sheria hii inapania kuharamisha umaskini kwa kuadhibu waraibu ambao ni wengi kwa idadi na wana kipato cha chini ilhali  walanguzi wakuu ambao ni mabwenyenye wakiwa na mwanya wa kutoadhibiwa.

Kwa mujibu wa mswada huo wanaopatikana na mihadarati chini ya gramu moja wanakabiliwa na faini ya shillingi millioni tano au kifungo cha miaka mitano au zaidi gerezani.

 

 

By reporter Preston Allan