HabariSiasa

KNUT kuandaa uchaguzi wa wanachama wake hivi karibuni…………..

Chama cha waalimu inchini KNUT kinatazamiwa kufanya uchaguzi wa kuwachagua viongozi wake tarehe 26 mwezi juni katika uwanja wa .

Akizungumza na wanahabari mjini Eldoret naibu katibu wa chama cha KNUT Hezbon Otieno amesema kwamba mipango yote imekamilika ya kufanikisha uchaguzi huo ikizingatia kanuni zilioko za kukinga maambukizi ya virusi vya corona.

Baadhi ya wanachama wa KNUT chini ya team change wanapendekeza kung`olewa kwa katibu wa chama hicho Wilson Sossion kwa kile wanachokitaja kama kufeli kutekeleza majukumu yake kwa wanachama wake na kufanya chama hicho kukosa ushawishi ikilinganishwa na miaka iliopita.

 

By Nicky Waita