HabariSiasa

Karisa Nzai asema ukabila ndio chanzo cha kudidimia kwa azimio la kuunda chama cha pwani……

Mwaniaji wa kiti cha ubunge katika eneo bunge la jomvu Karisa Nzai amesema ukabila ndio chanzo cha kudidimia kwa azimio la viongozi wa Pwani kuwa na chama chao.

Akizungumza katika kipindi cha sauti asubuhi, Nzai  amesema viongozi wa Pwani badala ya kushughulikia chama hicho kikamilifu na kuwaleta pamoja wananchi wa ukanda wa Pwani wao ni kueneza tu ukabila na chuki dhidi yao.

Wakati huo huo Nzai amesema kuwa viongozi hao wanataka pesa za kujifuruhahisha  pasi na kuangazia azmio la chama huku akidai kuwa pesa za chama sio tatizo.

 

By David Otieno