HabariMazingira

Serikali yatakiwa kumlipa mwanakandarasi huko Voi…..

Changatomo imetolewa kwa serikali ya kitaifa kupitia shirika la Kenya Railways kumlipa mwanakandarasi anayejenga upya shule ya wasichana ya Voi katika kaunti ya Taita Taveta baada ya shule hiyo kuathirika wakati wa ujezi wa reli ya SGR.

Kulingana na wazazi katika shule hiyo, ujenzi wa shule hiyo umechukuwa muda mrefu huku wakilaumu kutolipwa kwa mwanakandarasi huyo na serikali hali ambayo imelemaza pakubwa ujenzi wake.

Haya yanajiri huku wanafunzi wengi katika maeneo ya Kariako Maweni na Mlengwe viungani mwa mji wa voi wakitegemea pakubwa shule hiyo.

 

By Gladys Marura