HabariNews

Familia moja LAMU yaitaka serikali iwasaidie kumpata jamaa wao aliyetekwa nyara…….

Familia moja katika kaunti ya Lamu inataka serikali iwasaidie kumtafuta jamaa wao aliyepotea anayejulikana kama Yassir Ahmed mwenye umri wa miaka 43 wakiamini kwamba alitekwa nyara na watu wanaoshukiwa kuwa ni maafisa wa polisi.

Kulingana na familia yake, Yassir Ahmed hajaonekana tangu siku ya Jumamosi na inasemekana kuwa  gari lake lilisimamishwa na gari aina ya Land Cruiser yenye nambari za usajili za serikali alipokuwa anaelekea Lamu kutoka Mpeketoni eneo la Mkunumbi katika barabara kuu ya Lamu  mwendo wa saa kumi unusu.

Wanadai watu wenye sare za polisi walimchukua Yassir na kumwacha mke wake Yumna Ali,mwanawe pamoja  na dereva wao garini.

Ikumbukwe kwamba visa vya watu kutekwa nyara na kupotea kwa njia tatanishi vimekuwa vikiongezeka katika siku za hivi karibuni.

By Reporter